Utoaji wa ruzuku
Segal Family Foundation yanuia kuwa na uhusiano wa muda mrefu na mashirika kusini mwa Jangwa la Sahara yenye maono ya mbali. Timu yetu inatumia vigezo vya maono ya mbali kuchagua washirika wapya, na tunatumia mfumo wetu wa Active Partnership kuwaunga mkono. Lengo letu ni kuwaona washirika wetu wakiimarika na kuleta manufaa katika jamii zao, huku wakiwa katika nafasi ya kuendelea nza kazi zao hata pale ambapo udhamini wa Segal utakapofikia kikomo.


Tunavyochagua Washirika
Kwenye kutambua na kuchuja washirika watarajiwa, SFF inatumia mtazamo wa kijamii kwa kuwahusisha wataalam wenyeji. Mitandao yetu ni mipana, wakiwemo:
- Washirika wetu wa sasa na wa zamani tunaowaamini
- Vyama vya mashirika yasiyo ya kiserikali na jukwaa za jamii
- Ushirika wa sifa / mitandao ya rika
- Wafadhili wenzetu na mabalozi, hasa yale yanayotoa misaada ya kifedha


