
Grace Françoise Nibizi
Grace Françoise Nibizi ameolewa na ni mama wa wana wawili, mmoja wao anafanya kazi naye katika SaCoDé. Yeye ni wa 3 kuzaliwa katika familia ya watoto 10 na amelelewa na nyanya yake. Yeye kitaaluma ni nesi, lakini pia ana Shahada ya Kwanza katika Utawala wa Kijamii na Kiuchumi na uzoefu wa miaka mingi wa kufanya kazi katika mashirika kadhaa ya kimataifa ya kibinadamu na maendeleo: UNIFEM, UNDP, UNHCR, CRS na Umoja wa Ulaya. Alianzisha SaCoDé mnamo 2010 ili kuwawezesha wanawake na vijana wasiojiweza kudhibiti maisha yao na kuishi kwa heshima.